BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hamasa ya mafanikio ya leo.

Chochote kile unachokifanya, amua kukifanya kiwe kikubwa, hata kama sio leo, ila kwa baadae hakikisha kiwe kikubwa, kitu hicho kinaweza kuwa ni biashara, mahusiano au huduma, lakini amua kiwe kikubwa.

Ipo nafasi ya wewe kukifanya chochote unachokifanya kuwa kikubwa kabisa. Hakuna sababu ya kutokukifanya kuwa kikubwa na ukakiacha kibakie kuwa kidogo kwa miaka mingi, huko kutakuwa ni kudumaa sasa.

Inahitajika nguvu, nidhamu na juhudi kubwa ili kukifanya hicho unachokifanya kionekane kikubwa na kwa namna ya tofauti. Wapi unaposhindwa, wakati inawezekana kukifanya hicho unachokifanya kiwe kikubwa?

Ili ukifanye hicho unachokifanya na kikawa kikubwa, hakikisha ukijue vizuri, kiboreshe kila siku na kisha fanya kazi, nakwambia, ipo siku utaona matokeo yake na kitakuwa kikubwa kweli.


Post a Comment

0 Comments