Watu wengi wanatafuta sana njia rahisi ya mafanikio. Wanakuwa ni watu wa kutafuta kazi itakayowapa mamilioni leo, au wanatafuta maarifa ya ajabu yatakayo wafanya wawe matajiri ikiwezekana hata leo.
Watu hawa wanachosahau ni kwamba, wanatakiwa KUFANYA KAZI tena haswaa ili kufanikiwa. Njia ya mkato kufikia mafanikio haipo na kama ipo, kuna siku itakupoteza sana.
Washindi katika maisha, wao wanatafuta njia za mafanikio yao. Kila siku wanaweka juhudi, kila siku wanajitoa kwa kwenda hatua za ziada na mwisho wa siku hujikuta wamefanikiwa sana.
Unasubiri nini hapo ulipo, anza leo kutafuta njia ya mafanikio yako. Na achana na njia za mkato kama ambavyo watu wengine wameamua kuzifata au kuziishi wakiamini zitawafanikisha.

0 Comments