Hapo ulipo tuliza akili yako na angalia vitu vinavyokuzunguka. Angalia simu yako, nyumba yako, gari lako, kompyuta na vingine vingi, utagundua vitu vyote hivyo ni matokeo ya mawazo.
Na wanasayansi wanatuambia akili ya binadamu mpaka sasa, hakuna ambaye ameitumia hata kwa asilimia tano, lakini maajabu yake unayaona. Je, ingetumika kwa asilimia kumi?
Uzuri wake mkubwa ni kwamba huhitaji pesa, huhitajikuweka battery, kuchaji au kuweka mafuta, ili akili yako itumike, ni wewe tu kuamua unaitumiaje, na jinsi inavyotumika inatanuka tu.
Tupo kwenye dunia ya fursa nyingi sana, ni uamuzi wako kuitumia akili yako kwa jinsi wewe unavyotaka. Amua sasa kuitumia akili yako sana ili ikupe mafanikio makubwa.
NENDA UKAPIGE KURA....MAANA KURA NI HAKI YAKO

0 Comments