Kama tayari umeshafikia mafanikio ya aina fulani, acha kukubali tu kuishia hapo tu, amua kwenda juu zaidi, yaani usiridhike na hapo ulipo tu, utakwama.
Hiyo ikiwa na maana, mafanikio hayo uliyoyapata, yafanye yawe ghorofa, yafanye yawe ngazi ya kukusaidia wewe kufika juu zaidi au kufikia mafanikio mengine.
Ikitokea umeridhika na mafanikio yako, ukianza kurudi nyuma, usishangae kabisa, maana kinakuwa ni kitu ambacho umeamua mwenyewe sasa.
Unatakiwa ukumbuke, unahama kutoka falme hadi falme, utukufu hadi utukufu na mafanikio hadi mafanikio. Huu ni wakati wa kusonga mbele na si kuridhika.

0 Comments