Kati ya kosa ambalo hutakiwi kulifanya unapotafuta mafanikio, ni kule kuwashusha wengine chini, badala ya kuwasaidia. Amini hilo litakuwa ni kosa kubwa sana kwako kulifanya.
Unapowasaidia wengine, unajikuta na wao pia wanakusaidia wewe kufikia ndoto zako. Jaribu kuwasaidia watu wengi uone, kama na watu hao hawajakusaidia wewe kuzifikia ndoto zako.
Ila kwa jinsi unavyokwama kuwasaidia watu wengi na ndivyo na wewe unajikuta upo niia panda huwezi kufanikiwa tena, kwani apandacho mtu ndicho anachokivuna.
Wasaidie watu, wape wa vitu nawe utasaidiwa kwa kipimo kilichojaa na kuzidi hata kusukwa sukwa. Kama huamini katika hili, nikwambie tu, chukua hatua ya kusaidia watu na utaona matokeo yake.

0 Comments