Ni rahisi sana kuwa katika amani, kama mambo yako shwari. Lakini, amani hasa ya kweli inapatikana kama mambo yako hovyo hovyo, hapo ndipo amani ya kweli ilipo au inatengenezwa. Ni kipindi unachotakiwa kutulia sana.
Amani ya kweli, amani ya ndani halisi, haitegemei matukio ya nje, hata yawe mabaya kwa namna gani. Amani ya kweli inategemea mwelekeo wako, kujiamini, malengo yako na imani yako.
Hiyo ina maana gani, ni kwamba, haijalishi kitu gani kinatokea kwenye maisha yako, lakini unatakiwa uwe na amani. Jifunze kuangalia uzuri wa fursa zinazotengeneza maisha yako.
Amani ya kweli ni mwanzo wa maisha bora, busara na mafanikio makubwa kwako leo na kesho.

0 Comments