Tupo na tunaishi kwenye ulimwengu wa kelele nyingi sana, ikiwa pamoja na habari, mitandao ya kijamii na kelele nyinginezo kedekede. Na kwa sababu hiyo, tunajikuta tunakosa muda wa kukaa na kufikiria maisha yetu kabisa.
Inatakiwa uelewe hivi, tunapoamua kukaa nje ya makelele, tunajifunza vitu vingi sana na kujitambua sisi uwezo wetu, na nguvu zetu tulizo nazo. Kelele moja kwa moja zinatoa utulivu huo.
Kelele nyingi za dunia, zinatupotezea nguvu za kufanikiwa kwetu na mafanikio kwa ujumla. Kwa hiyo, jukumu letu ni kukaa mbali na makelele ili kupata utulivu wa mafanikio.
Kila utakapotulia, utashangaa, unapata uwezo na nguvu nyingi za kukufanikisha. Hakikisha unatafuta angalau siku chache kwa wiki kuvuta utulivu.

0 Comments