Kati ya kanuni rahisi ya kuweza kukusaidia kupata chochote unachokitaka ni kanuni ya KUULIZA/ASK. Kwa kutumia kanuni hii utapata vingi unavyovitaka.
Ni ahadi ya biblia ya kwamba, ombeni nanyi mtapewa na hilo liko wazi na sahihi.
Ni jukumu lako kuulizia oda kwa wateja wako ili uzipate kwa uhakika oda hizo.
Ni jukumu lako kuulizia punguzo, na punguzo hilo ukiliomba utalipata pia.
Ni jukumu lako kuulizia kazi unayoitaka, na kazi hiyo utaipata, kwa sababu umeiomba.
Chochote unaweza kukiuliza au kukiomba na utakipata bila tabu yoyote ile.
Watu wamefundishwa toka wakiwa wadogo,wakiombwa kitu watoe, hivyo unatakiwa pia na wewe kuomba ili ufanikiwe.

0 Comments