Nguvu na uimara katika maisha yako, hautokani na wewe kufanya mambo mepesi, bali unatokana na wewe, kupitia katika nyakati ngumu, na zenye changamoto kubwa sana.. Hapo ndipo uimara na nguvu yako hupatikana.
Wabeba vyuma wanajua hili, kila ukibeba vyuma vizito misuri inatanuka, hivyo hilo ni fundisho kwamba kila changamoto inakufanya iwe imara sana na mwenye nguvu.
Changamoto zinakuwa zinatupa kitu fulani cha kufanya na kukua. Kubali kukabiliana na changamoto ngumu, ipo fursa ndani yake ambayo wewe huioni, lakini ipo.
Changomoto na nyakati ngumu,ni njia ya wewe kuweza kufanya kitu kipya, kukua kiakili, kutengeneza busara, kuona fursa upya na kufanikiwa, TAFAKARI.

0 Comments