Njia pekee ya kupata pesa, ya kupata umaarufu na ya kupata kile unachokihitaji inapatikana kwa wewe, kuwapa watu vitu wanavyovihitaji. Ukiwapa watu kile wanachohitaji kila kitu utakipata tena kwa uhakika.
Uwe unataka utajiri, afya au chochote kile, ukifanikiwa kuwapa watu vitu wanavyovihitaji hayo yote utayapata na tena na kuzidi. Hii ndio siri ya kupata kila kitu maishani mwako.
Kuna wakati tena wape watu vitu wanavyohitaji hata kabla wao hawajajua wanahitaji vitu hivyo, utapata pesa mpaka utashangaa. Usipowapa watu vitu wanavyohitaji, utapishana sana na pesa kila wakati.
Uhakika wa maisha yako, upo kwa wewe kuwapa watu vitu wanavihitaji, yaani 'give people what they want'* na sio kinyume cha hapo, utakosa mengi.

0 Comments