Hebu jiulize, unawezaje kutoa yale yaliyobora kwa wengine. Jibu ni rahisi tu, ni kwa wewe kuamua kufanya yale yaliyobora kwako. Kwa kufanya yale yaliyobora kwako, basi hata kwa wengine unaweza kutoa yaliyobora.
Waangalie walimu, waajiri, ma afisa mauzo, hawa ni watu wanaojitahidi sana kutoa yale yaliyobora kwa watu wao, pia wanafunzi, waajiriwa na wateja hujitahidi kutoa yaliyobora kwa wale wanaowahusu.
Elewa kwamba, maisha yanakuwa bora sana kwa kila mtu, ikiwa kila mtu ataamua kufanya yaliyobora kwenye maisha yake. Ukifanya mambo kwa ubora kwako, basi hata kwa wengine ni rahisi kuwafanyia.

0 Comments