BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jifunze haya kutoka kwenye kitabu cha I Will Teach You to Be Rich: No Guilt. No Excuses. Just a 6-Week Program That Works kilichoandikwa na Rammit Seth

 


Leo nimekuleta mambo matano (05) ya kujifunza  kutoka kwenye kitabu cha I Will Teach You to Be Rich: No Guilt. No Excuses. Just a 6-Week Program That Works  kilichoandikwa na Ramit Sethi.

1. Mwandishi wa kitabu hiki Ramit Seth anasema kuwa pesa ni itumike kama kifaa kwa ajili ya kuweza kutimiza malengo mbalimbali uliyojipangia. Pia anasema pesa yeyote unayoipata basi iwekee mikakati ya kujifanya pesa hiyo ijazalishe na si kuitumia pasipo pesa hiyo kuwa mwendelezo.

2. Tengeneza mikakati mizuri ya pesa: kitabu kinafundisha namna sahihi ya kuweka mifumo endeshi ya fedha zako. Kila mtu ni lazima awe na mfumo wa kuweka akiba, mfumo wa kuwekeza na mfumo wa kulipa bili mbalimbali. Mifumo hiyo huitwa namna  sahihi ya kutunza fedha, ambapo ni lazima ugawe matumizi hayo kwa kuzingatia asilimia hii itategemeana na kipato chako.

3. Wekeza kwa ajili ya wakati ujao, na si kwa ajili ya wakati wa sasa:mwandisi Seth anasema kuwa weka kipaumbele kwa ajili ya uwekezaji aa fedha zako. Uwekezaji huo ni ule ambao matokeo yake hautauaona sasa bali wakati ujao. Uwekezaji huo ni ule ambao huchua miaka kadhaa ndipo uone matunda ya kile ulichowkeza.

4. Epuka madeni yasiyokuwa na ulazima. Kitabu kinatukumbusha namna ya kutengeneza mifumo ambayo si rafiki hasa pale linapokuja suala la madeni. Mwandishi anataka tuepuke madeni yasiyokuwa na tija kwa sababu wakati mwingine madeni chanzo kikubwa cha upotevu wa pesa zetu. Ili kuepuka madeni hayo basi  hakikisha unaweka malengo vya kifedha (financial goals).

5. Chukua hatua pia epuka kuwa mghairishaji wa mambo: Mwandishi Sethi anasema kuwa ni lazima uwe mtu wa kuchukua hatua kwenye masuala ambayo yanahusu malengo ya kifedha kuliko kuwa mtu wa kughairisha mambo. Kama kuna jambo linahusu suala la pesa liweke kwenye matendo ili uweze kutengeneza mazingira ya kupata pesa zaidi.

Mpaka kufikia hapo naamini kuna jambo kubwa umejifunza. Nikutakie siku njema na mafanikio mema.

Imeandikwa na fundi, mshona maneno Benson chonya.

Post a Comment

0 Comments