BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jifunze haya kutoka kwenye kitabu cha kitabu cha 18 minutes Find Your Focus, Master Distraction, and get the right things done cha Peter Bregman.

 



Masomo 7 utakajifunza kutoka kwenye kitabu cha 18 minutes  Find Your Focus, Master Distraction, and Get the Right Things Done kilichaondikwa na Peter Bregman.

1. Pata muda wa kupumzika. Mwandishi Peter anasema kuwa kila unachofanya basi tenga muda wa kupumzika hasa pale unapokuwa umechoka. Unapopumzika inakusaidia kutuliza akili na kuongeza nguvu pia ya kufanya jambo fulani kwa ukubwa zaidi. Hivyo ipo faida lukuki ya kupumzika, hivyo usifanye kazi mfululizo pasipo kutenga muda wa kupumzika.

2. Ijue nguvu uliiyonayo. Tunafahamu kuwa kila mwanadamu ana uwezo na udhaifu fulani ndani yake. Pamoja na hayo yote basi unapofahamu udhaifu wako, basi jitahidi uweze kubadili udhaifu huo uwe katika uwezo, si uwezo tu bali uwe uwezo chanya wa kufanya jambo lenye mantiki fulani. Mwandishi wa kitabu hiki anahamasisha watu kutumia ujuzi wenye manufaa ili kufanya vitu chanya zaidi.

3. Usipambane na madhaifu yako. Kupambana na madhaifu yako muda mwingi ni kupoteza muda hii ni kwa mujibu wa mwandishi Peter. Kitabu kinatuasa tuweze kufanya yale yaliyo bora ambayo yana mchango mkubwa sana katika kuleta mabadiliko makubwa kwenye kile tunachokifanya. Madhaifu yetu tukiendelea kuyabeba yanatufanya tuwe dhaifu pia wakati mwingine kuwa waoga wa kuthubu kwenye kufanya maamuzi ya kiutendaji.

4. Jifunze kuwa tofauti. Kila kitu ili kikupe matokeo tofauti na watu wengine wanayoyapata basi jifunze kuwa wa tofauti. Kaa chini na utafute upekee wako, huo ndiyo utakaoleta utofauti na watu wengine. Pia ukishaujua upekee wako, basi wekeza nguvu kubwa kwenye upekee huo. Ukifanikiwa kwenye jambo hilo mambo mengi utaona jinsi yatakavyokuletea matokeo chanya zaidi.

5. Fanya kile unachokipenda. Mafanikio yamejificha kwenge kona hiyo ya kufanya unachokipenda. Ukifanya unachokipenda utapata moteko makubwa sana kwa sababu ya msukumo wa kufanya jambo utakuwa unaotoka ndani yako. Kukipenda kitu ndiyo siri ya mafanikio halisi unayoyataka.

6. Maajabu ya dakika 18. Mwandishi anasema dakika 18 zina uwezo mkubwa wa kufanya maajabu makubwa sana. Peter anashauri upange ratiba fupi kila siku ya dakika 18. Dakika hizi ni za kufanya maajabu. Dakika hizi ziwe kwenye ratiba yako ya kila siku, ambapo itakulazimu kufanya jambo moja muhimu. Ukifanya hivyo kwa mfululizo utaona namna ambavyo mambo yatakavyobadilika zaidi kwako.

7. Kuwa bosi wa muda wako. Usiwafanye watu wengine wakupangie ratiba zako, bali wewe ndiye unatakiwa kupanga namna sahihi ya kutumia muda wako. Jifunze kusema hapana kwenye mambo yaisyokuwa na maana hasa yale yanayokupezea muda. Kuwa mtu wa vipaumbele, epuka kufanya mambo ambayo hayakuwa kwenye ratiba zako. Heshimu muda na utumie vizuri, kwani wahenga walisema muda ni mali.

Kwa nukta hiyo naamini kuba jambo umejifunza, nikulike kwenye uchambuzi wa kitabu kingine siku ya jumapili ijayo, hapa hapa mafanikio app muda wa tisa alasiri.

Ukiniita Afisa Mipango Benson Chonya Nitaitika, kumbuka kuanza na neno afisa mipango😃

Post a Comment

0 Comments