Ili uweze kufanikiwa kifedha unapaswa kujifunza kutofautisha kati ya matumizi ya lazima na matamanio.
Wengi wetu tunapoteza fedha zetu nyingi kwenye vitu vya matamanio zaidi.
Tunafanya matumizi kwenye vitu ambavyo wakati mwingine hatuna hata uhitaji navyo ila tunafanya hivyo kwa sababu tunaendeshwa na hisia za matamanio tu.
Unakuta mtu hakupanga kununua kitu fulani ila kwa sababu mtu huyo anaendeshwa na hisia tu za matamanio unakuta kanunua kitu hicho pasipo kupanga.
Kuendelea kufanya kitu hiki si sawa hata kidogo kwa sababu kama utaendelea kufanya hivyo hutaona thamani ya pesa ambazo hukatisha mbele yako, hii kwa sababu kila fedha itakuwa inapitiliza tu kwenye matumizi yasiyokuwa na maana.
Kama nilivyosema hapo awali kuwa wengi wetu huendeshwa zaidi na hisia za matamanio na kila kipato chetu kinavyoongezeka pesa hizo huishia kwenye kununua vitu hivyo visivyokuwa na ulazima.
Pia ukweli pekee usioufahamu kuhusu vitu vya matamanio ni kwamba huwezi kuvitimiza vyote kwa mara moja. Kila unapotimiza hiki kinakuja kitu kingine ambacho kinakuwa ni kizuri zaidi ya kile ulichonunua mwanzo.
Ikumbukwe kuwa hata uwe na fedha nyingi kiasi gani ila ukiwa unaongezwa na akili ya matamanio hakuna kitu cha maana utakachofanya, kwa sababu pesa yako yote itakuwa inaishia kwenye mambo hayo ya kimatamanio.
Sasa ili tuweze kufanikiwa kifedha ni muhimu sana kupunguza matamanio mengi yasiyokuwa na ulazima ili tuweze kufanikiwa. Fanya matumizi ya fedha kwa kupanga na si kwa kurupuka tu.
Nb: Pesa ipo kwa wale wanaoijua sheria zake na kuzifuata
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya.
0747-030303
0 Comments