Kanuni pekee ambayo unaweza kuitumia ili uweze kuona kila thamani ya fedha inayokatisha kwenye mikono yako ni kuwa na ukomo katika matumizi.
Unapokuwa na pesa kuwa makini sana matumizi yako. Usitumie fedha nyingi kwa sababu eti unazo fedha hizo au una uhakika wa kupata tena nyingine.
Kama umezoea kutumia shilingi mia tano kwa siku kwenye kipato chako cha shilingi elfu mbili, basi jitahidi sana hata kipacho chako kikiongezeka matumizi yako yabaki yale ya shilingi mia tano labda vinginevyo kuwe na ulazima wa wewe kuongeza matumizi yako.
Nimesema hivyo kwa sababu pesa mara nyingi pesa huwa smzina makelele za kumkumbusha mmliki wa fedha hizo kwamba afanye matumizi, na kelele hizo hutokea hasa pale mtu huyo kipato chake kinapoongezeka.
Hivyo njia pekee ya kuthibiti matumizi yako hasa pale kipato chako kinapoongezeka, ni kuwa na ukomo wa kufanya matumizi yako. Si kila kitu lazima ukinunue, si kila safari lazima usafiri, si kila mtindo wa maisha lazima uishi, si kila gari la thamani lazima uwe nalo.
Kuwa na ukomo wa matumizi yako itakusadia sana kwa kuepuka kufanya matumizi au matanuzi yasikyokuwa na ulazima
Nb: Fedha ipo kwa wale wanaoijua sheria zake na kuzifuata.
Imeandikwa na afisa mipango Benson Chonya.
0747030303
0 Comments