Ili uweze kuishi maisha yenye furaha na amani tele ndani yako hususani suala la kufanya matumizi sahihi ya pesa, unatakiwa kuchunguza namna unavyoishi na unavyofanya matumizi yako ya kila siku.
Wengi wetu hatuna tabia ya kuandika matumizi tunayotaka kuyafanya kwa siku husika, kitendo ambacho kinatupelekea kufanya matumizi ambayo wakati mwingine hayana ulazima wowote wa sisi kuweza kufanya hivyo.
Jukumu pekee ambalo unatakiwa kulifanya ni kuhakikisha unaandika mahitaji yako kisha angalia ni yapi ya muhimu na yapi si ya muhimu kuweza kuyanunua.
Yale ambayo si ya lazima ni muhimu sana uweze kuachana nayo na yale ambayo ni ya muhimu basi unaweza kuyatekeleza.
Anza mara moja utaratibu huu wa kuandika yale unayoyahitaji kununua kupitia pesa yako ili kuepusha kufanya matumizi kwenye yale yasiyokuwa na ulazima. Epuka kununua kitu ambacho hukupanga.
Imeandikwa na afisa mipango Benson Chonya.
.png)
0 Comments