Kama ilivyo ule usemi maarufu usemao "hatma ya maisha yako ipo mikononi mwako" basi hata jukumu la kupanga bajeti yako ipo ndani ya uwezo wako.
Kumpa jukumu hilo la kupanga bajeti yako lifanywe na mtu mwingine ni sawa na kumwambia punda abebe mizigo anayotaka yeye.
Kwa akili yako unafikiri ukifanya hivyo je punda huyo atafanya kama wewe unavyotaka? Jibu ni hapana bali punda huyo atabeba mizigo kulingana na yeye anavyotaka.
Kwa muktadha huo utaona ni kwa namna gani jukumu la kupanga bajeti yako linatakiwa lianzishwe na wewe ili mambo mengine yaende kama vile utakavyo wewe.
Kupanga bajeti yako ni muhimu sana, kuishi bila kuwa bajeti ni sawa kuanzisha safari ghafla huku ukiwa huna uelekeo ya kule uendako ni lazima utapotea tu.
Ili usipotee ni muhimu kila mmoja wetu kuwa na bajeti yake ambayo anakuwa anaipanga yeye mwenyewe.
Kuwa na bajeti ni muhimu sana kwa sababu hii itatumika kama ramani ambapo itakusaidia sana kwenye kufanya matumizi na kujua hela zako zinatumika wapi zaidi.
Je ni kwenye matumizi ya lazima au kwenye matumizi yasiyokuwa na ulazima? Panga bajeti ili kujua matumizi ya lazima na yale siyo kuwa na lazima.
Usifanye matumizi ya pesa kama yapo nje ya bajeti yako.
Imeandikwa na afisa mipango Benson Chonya
.png)
0 Comments