Wengi wanaishi maisha kutokana na kuiga, mtu akiona mtu mwingine ana simu nzuri, gari nzuri au kitu chochote kizuri naye anatamani awe na kitu hicho pasipo kuangalia uwezo wake.
Aina hii ya mtindo wa maisha ndipo niporejea kusema wengi wetu tunaishi mitindo ya maisha isiyokuwa rafiki kwa sababu mwisho wa siku huwa tunaambulia maumivu makali sana kwani huwa tumekuwa tumefanya maamuzi ya kununua vitu ambavyo hatukupanga kufanya hivyo.
Kitendo ambacho hufanya mwisho wa siku tusione thamani fedha zinazopita mikononi mwetu. Sasa ikiwa unataka kubadili aina ya maisha unayoishi na kuona kila thamani ya pesa unayoipata basi unatakiwa sana kuishi kulingana na uwezo wako, pia ishi kulingana na mtindo wa maisha unaokufaa.
Acha kuishi maisha ya kuiga kwani ukiendelea kufanya hivyo hutaona thamani ya fedha zako kwani utakuwa unafanya matumizi ambayo hukupanga kufanya hivyo.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya.
.png)
0 Comments