Hapa kuna masomo 5 kutoka kwenye kitabu "Build Your Dream Network: Forging Powerful Relationships in a Hyper-Connected World" kilichoandikwa na J. Kelly Hoey:
1. Uhusiano na watu wengine ni muhimu. Mwandishi Hoey anasisitiza umuhimu wa kujenga uhusiano wa kweli kama msingi wa kazi yenye mafanikio. Ambapo anasisitiza wasomaji wa kitabu hiki kujenga mahusiano mazuri na watu wengine kwani husaidia sana kujenga heshima baina yetu pia husaidia kushirikiana katika kazi mbalimbali ambapo husaidia kuongeza maslai katika jambo fulani.
2. Unapoungana na watu wengine husaidia sana kuweza kukuza mtazamo sahihi juu ya kujua fursa mpya zinazopatikana kwenye eneo husika kuliko kubaki wewe mwenyewe pekee. Ipo nguvu kubwa sana ya hasa pale utakapoamua kujenga mtandao na watu wengine kwani hukusaidia kujua mambo yale ambayo hapo awali ulikuwa huyafahamu kabisa.
3. Kiatbu hiki pia kinaangazia kuwa wakati mwingine tumia teknolojia ili uweze kupata fursa nzuri ya kuweza kutengeza mitandao ya kuweza kufahamiana na watu mbalimbali. Wapo baadhi ya watu wanafanya mambo makubwa hii yote inatokana na kufamiana na watu mbalimbali kutoka kwenye mitandao ya kijamii. Matumizi sahii ya majukwaa kama vile linked, facebook, mtandao wa twitter ambao sasa unafamika kama X, instagram na mitandao mingine. Hii ni njia nzuri ya kuweza kufahamiana na watu wengine ambao watakusaidia kwenye manufaa zaidi.
4. Unapojenga mtandao wako hakikisha unakuwa ni ndani ya malengo yako, mwandishi wa kitabu hiki anasema epuka kutoka nje ya malengo yako. Malengo yako ndiyo hutoa muongozo aina ya watu unatakiwa kuwa nao katika mtandao wako. Pia mwandishi anaweka mkazo wa juhudi na ufanyaji wa kazi zako ili uweze kupata watu sahihi.
5. Unapojenga mtandao na watu tofauti tofauti mwandishi anashauri basi kuwa ni vyema kuendelea kuwasiliana mara kwa mara ili muwezee koboresha mahusiano hayo mliyoyatengeneza. Mawasiliano mliyoyatengeneza ni muhimu yaendelezwe kwa sababu msipoendeleza mahusiano hayo itakuwa sawa sawa na bure.
Nb: Kujenga mahusiano haya ni lazima yawe ni ya kutimiza malengo ya maisha na si vingivyo, rudia sentesi hii ili uweze kuelewa vizuri. Ipo nguvu kubwa ya kujenga Dream Network lengo ikiwa ni kufungua fursa mpya za maendeleo ya kazi na ukuaji wa mtu binafsi au jamii kwa ujumla.
Imeandikwa na Benson Chonya.
Tukutane kwenye uchambuzi mwingine jumapili ijayo hapa hapa mafanikio app.
.jpeg)
0 Comments