BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Acha mara moja tabia hii maishani mwako.

Watu wengi wanashindwa kufanya vizuri katika maeneo wanayoyafanyia kazi kwa sababu ya kukosa kwao uwezo wa kujiamini. Wao wamekubwa na tatizo kubwa la kujilinganisha wao kwenye yale wanayoyafanya na  watu wengine wanaofanya mambo kama yale wanayofanya wao.

Kwa kitendo hiki kimesababisha watu hao kujiona kama vile hawajui sana wakijilinganisha na watu wengine. Kitendo hiki cha kujilinganisha na wengine kimesababisha watu wengine wajione hawana thamani na uwezo wa kufanya vizuri zaidi.

Kwa muktadha huo, unachopaswa kuelewa ni kwamba wakati mwenyezi Mungu alipomuumba mwanadamu alimpa kila mtu uwezo wake binafsi uwezo ambao huwa haufanani na mtu mwingine, kama ndivyo hivyo kwanini uendelee kujilinganisha na wengine.

Tambua kitendo ambacho unakifanya cha kujilinganisha wewe na watu wengine kitakufanya ujione kama vile hujui na wakati mwingine kitakuondelea kabisa uwezo wako wa kujiamini. Hivyo unatakiwa uache mara moja tabia yako ya kujilinganisha na wengine kwa sababu unajiua wewe mwenyewe pasipo kujua.

Na ndiyo maana upo usemi mmoja unasema “Samaki hawezi kupanda juu ya mti, gedere hawezi kukimbia kama farasi, baadhi ya ndege pori hawewezi kuogelea. Hii ikiwa na maana kila mmoja ana uwezo wake, kutokana na uwezo wake aliyeoumbwa nao wa kufanyia kazi na kufurahia maisha yake. Hivyo furahia uwezo ulio nao acha kujilinganisha na wengine kwa sababu kila mmoja ana uwezo wake.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments