BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hivi ndivyo muda unavyoweza kukupa mafanikio.

Yupo mwana falsafa mmoja aliwahi kusema kwamba (time is Money) kwa kibantu akiwa na maana ya kwamba muda ni mali. Hilo lipo wazi kabisa  kama unataka kufanikiwa katika maisha yako kwa namna yeyote ile basi unatakiwa kutumia vyema muda wako.

Unachopaswa kufanya ni kukikisha kila siku ithamini siku yako kwa kufanya yale yaliyo ya muhimu kwa sababu kama utashindwa kufanya jambo la msingi leo, kumbuka kwamba siku hazigandi bali zinazidi kwenda, na muda nao unazidi kuyoyoma hivyo usipoafanya leo unaweza usipate muda mwingine wa kuweza kufanya tena. 

Katika matumizi ya muda hakikisha kila siku una kuwa na ratiba yako ya binafsi ya kufanya mambo yako binafsi, usifanye mambo kama hayakuwepo kwenye ratiba zako. Pia kila wakati tenga muda kwa ajili ya kujifunza mambo mapya katika eneo ambalo unafanyia kazi.  

Unapaswa kutenga muda wa kujifunza kwa sababu watalamu wa mambo wanasema kama utatenga  muda wa saa moja kila siku katika kujifunza kitu kipya katika eneo lako la kazi basi ndani ya mwaka mmoja utakuwa ni mtalamu (expert) sana wa jambo hilo.

Kumbuka, kila siku unapaswa kufanya taathimini kwa kuona ni kwa namna gani umeutumia vyema muda wako katika kufanya yale yaliyo ya msingi na yenye faida kwako kwa sababu muda ni mali.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments