BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Aina za uvivu katika maisha .

Katika maisha kuna aina mbili za uvivu ambazo, ni uvivu wa kufikiri na uvivu wa kutenda. Aina hizi za uvivu ndizo zinazorudisha watu wengi sana kwenye mambo wanayoyafanya.  Kwa mfano mtu anataka kufanya jambo fulani ila uwezo wake wa kufikiri huwaza juu juu katika jambo hilo pasipo kufikia mwisho na kuacha jambo hilo pasipo kulipatia hatima yake.

Au unaweza kukuta  mtu maisha yake yanaongozwa na uvivu wa kutenda jambo fulani, kwa mfano unakuta mtu kila akitaka kutenda jambo fulani basi yeye hujikuta anaacha kufanya jambo hilo au hata kama akilifanya jambo hilo halifanya kwa kiwango kinachostahili bali yeye anafanya juu juu tu, na kitendo hiki kinamfanya mtu huyo awe na maisha ya kawaida miaka nenda miaka rudi.

Aina hizi za uvivu ndizo zinazowakwamisha wengi, Ikiwa umechoshwa na hali ya ugumu wa maisha yako unayoishi kwa hivi sasa ni vyema ukaamua sana kuanza kupunguza uvivu wako wa kufikiri na uvivu wako wa kutenda. 

Nimesema uanze kujifunza kupunguza aina hizo za uvivu kwa sababu siyo kitendo cha siku moja, hivyo unatakiwa uanze kuchua hatua kidogo kidogo mwisho wa siku itabadilika na kuwa ni tabia yako na utaona mabadiliko makubwa sana katika maisha yako.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments