Hakika! Kitabu cha "The Art of Laziness" kinaweza kutoa mawazo ya kufurahisha na ya kinahusu kufanya mambo kwa njia ya kiufundi zaidi pia kitabu hiki kinafundisha kwa kina namna ya kuondokana na uvivu katika kazi.
Hapa kuna mambo saba ya kujifunza kutoka kwake:
1. Kipaumbele cha kazi zenye tija.Watalamu wa mambo wanasema kuwa unaweza kufikia malengo mengi zaidi kwa kufanya kazi kwa akili badala ya kufanya kazi kwa bidii tu. Ili ufanye kazi kwa akili ni lazima uwe mtu mwenye vipaumbele, vipaumbele ni kuwa na mpangilio katika kazi zako yaani ni lazima ujue kuwa ikitoka kazi hii inafata kazi hii, ukiwa mtu wa namna hii utakuwa ni mtu mwenye mafanikio na uvivu wa kazi utajitenga nawe.
2. Kujifunza kubadilishana mawazo na watu wengine. Wakati mwingine unakuwa mvivu wa kufanya yale yaliyo na tija kwa sababu umekuwa ukiamini katika mawazo binafsi. Lakini ukweli ni kwamba hakuna mawazo binafsi yatakayokupa mafanikio ya moja kwa moja bali unapaswa kushirikiana na wengine kwenye kubadilisha mawazo. Ipo nguvu kubwa ya kiutendaji utakayoipata endapo utaamua kubadilishana mawazo na watu wengine.
3. Fanya jambo kidogo kidogo. Waswahili walisema haba na haba hujaza kibaba hivyo ni jambo jema sana kuelewa kuwa unapofanya kidogo dogo akili hugeuza jambo hilo na kuwa tabia ambapo ipo siku litakuwa jambo kubwa litakalokusaidia kupata matokeo makubwa zaidi. Usidharau kufanya jambo dogo kila siku kwa sababu hili ni jambo jema sana litakalokusaidia kupata matokeo kwa ukubwa zaidi na kuondokana na tabia ya uvivu pia.
4. Tenga muda wa kupumzika. Kufanya kazi kwa mfululizo pasipo kupumzika wakati mwingine kunakufanya usipate matokeo sahihi. Hivyo unapaswa kutenga muda wa kupumzika hasa pale unapoona akili imechoka na haiwezi kuendelea kufanya kazi. Kila wakati unapaswa kuelewa kuwa kupumzika ni muhimu sana kwa sababu huongeza sana ufanisi kwenye kazi zako.
5. Jifunze kupuuza mambo yasiyo muhimu. Si kila mfuko unafaa kuwekwa pesa, hapana mifuko mingine imetoboka maana yake si kila jambo unatakiwa kufanya mambo mengine unatakiwa kuyapuuza. Mambo yenye manufaa zaidi kwako yafanye na yale yasiyokuwa na manufaa kwako yapuuze. Kufanya mambo yasiyo na muhimu ni matumizi mabaya ya muda hili ni lazima ulifahamu.
6. Kufurahia maisha na kazi yako. Ukifurahia kile unachokifanya na kukipenda utaondokana na tabia ya uvivu na kupata matokeo sahihi. Pia anza sasa kwa kubadili mtazamo wako kwa kuongeza ubunifu katika kazi ili uweze kuwa bora zaidi ya jana.
Kitafute kitabu hiki ili uweze kujipatia mwenyewe wingi wa maarifa yanayopatikana kutoka kwenye kitabu hiki.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya.
Tukutane jumapili ijayo kwenye uchambuzi wa kitabu kingine hapa hapa mafanikio app
.jpeg)
0 Comments