BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Kabla ya kuanzisha biashara yeyote ile fanya haya.

Kabla hujaanzia biashara yeyote ile ni vema ukaangalia kwanza soko linataka nini? Ni muhimu kangalia jambo hili kwa sababu kuna wakati mwingine unaweza kujikuta unalazimisha wateja wako kununua vitu wasivyovijua.

Kumbuka tunaposema kuangalia soko lako linahitaji nini tunamaana ya kwamba kuangalia wateja kile wanachohitaji. Ni vigumu sana kuanzisha biashara yenye mafanikio pasipo kufanya uchunguzi wa kile wateja wako wanachokitaji. 

Pia upo usemi usemao ni vema ukajifunza kuanzia sokoni kabla ya kuanzisha biashara yako ili kujua ni nini wateja wanachotaka kisha wewe kuweza kuwasogezea wateja hao bidhaa au huduma fulani. Pia mbinu hii ya kuanzia sokoni ni mbinu ambayo huwa inatumika pia ya kutambua fursa mahali unapoishi.

Hivyo kwa chochote kile unachokifanya aidha ni biashara au kitu kingine, ni muhimu sana kuweza kuanzia sokoni, kwani unapoanzia sokoni utajua nini wateja wanachokitaka kisha wewe kuwasogezea watu hao bidhaa au huduma hiyo.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments