Kila siku inakuja na mshangao wake. Kuna siku ambayo inakuja na kukufanya ucheke, ufurahi na kuna siku inakuja inakufanya ulie, uhuzunike, hiyo yote ni mishangao ya kila siku.
Ikitokea kwako umelia sawa, ikitokea kwako umeshangilia pia sawa, hiyo yote ni mishangao. Kikubwa kwako unatakiwa kujiandaa, na kukutana na mshangao wa aina yoyote ile.
Hakuna siku ambayo inakuja bila mshangao, kila siku inakuja na mshangao wake na wa kipekee. Hutakiwi tena kuendelea kushangaa mishangao hiyo, weka akilini na jiandae tu.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.

0 Comments