BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Amaua kuitumia leo yako vyema kwa manufaa.

Njia pekee itakayokusaidia kuweza kufanikiwa katika maisha yako ni pamoja na kupanga kesho yako leo.  Ni muhimu kupanga kesho yako leo kwa sababu muda unazidi kwenda na pindi utakaposhindwa kupanga leo yako vyema ni kwamba utashituka siku zinazidi kwenda na haujafanya jambo lolote la maana.

Wapo baadhi ya watu wao wameajiriwa na wanaendelea kujisemea na mioyo yao kwamba pindi watakapostafu ndipo watakapoanza kufanya vitu vyao binafsi. Ukweli ni kwamba kama umeshindwa kufanya mambo yako leo vyema basi sahahu kuhusu kufanya jambo hilo kesho. 

Unachopaswa kuelewa ni kwamba unapaswa kuithamini leo yako vyema, hii ni kwa sababu mataumizi ya leo yako vyema, inatengeneza kesho yako iliyo njema na yenye mafanikio tele ndani yako. Amua sasa kuitumia leo yako vyema kwa kufanya yaliyo ya muhimu ili kesho yako usije ukajuta. Kumbuka, kinachowezekana leo kisingoje kesho.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments