BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jambo hili linawachelewesha watu wengi sana.

Watu wote wenye tabia ya kulalamika juu ya hatma ya maisha yao, watu hao mara nyingi huwa wanaishi maisha ya kawaida. Wanaishi maisha ya kawaida kwa sababu wao wanadhani kwamba mtu fulani amesababisha wao kuwa hivyo. Sijui huenda ikawa ni kweli kwa namna moja ama nyingine.

Maneno ya kusema baba amesababisha kuwa hivi, mara shangazi ndiyo chanzo cha haya yote au serikari ndiyo imesabibisha mimi kuwa hivi. Maneno ya kuendelea kulaumu bila kutafuta muafaka wake ni kuendelea kujichelewesha mwenyewe kufikia katika kilele cha mafanikio yako.

Ukweli uliyo wazi ni kwamba haijalishi ugumu unaopitia hivi sasa, pia haijalishi kwamba nani alikukwamisha kufika mahali fulani  au kutekeleza jambo fulani. 

Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha yale yote ambayo yamepita katika maisha yako haitakiwi kuendelea kuyabeba kwa sababu pindi utakapoendelea kuyabeba  yatakukwamisha kufikia malengo yako. 

Yote uliyokwisha kuyapita yabaki kuwa historia huku ukiendelea kupamabana na mambo yako binafsi katika kutenda yale yaliyo ya muhimu ambayo yatakusaidia kuweza kupiga hatua za mafanikio yako,  punguza kulaumu kwa sababu kulalamika bila kutafuta suluhu hakutakusaidia kwa lolote lile.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments