BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Epuka hili unapotaka kufanya biashara.

Miongoni jambo muhimu unalopaswa kulizingatia kama unataka kufanya biashara yeyote ile ni kwamba usiwekeze kwenye biashara ambayo huijui vizuri. Ni muhimu kulizingatia hili kwa sababu asilimia 90 ya biashara ambazo hufa mara baada ya kuanzishwa ni kwamba waliozianzisha biashara hizo  walikuwa hawazijui vizuri biashara husika.

Zipo biashara nyingi ambazo si vema kuingia mwili mzima mzima katika kuzifanya biashara hiyo kama huijui vyema. Biashara kama cryptocurrency, biashara ya hisa, Network marketing, real eastate na nyinginezo nyingi si biashara za kuanza kufanya kabla huzijua vyema.

Si vyema kuanza biashara hizo kichwa kichwa kwa sababu zinahitaji uweze kujifunza kwa muda mrefu ili uweze kuzifanya. Biashara nyingine zinakutaka usome vitabu hata kumi ili uweze kuzielewa vizuri kabla ya kuanza kuzifanya. Biashara hizo zinakutaka usome hata vitabu kumi kwa sababu ili uweze kujua fursa na changamoto zinazopataikana kwenye biashara husika.

Usikurupuke kuchukua maamuzi eti kisa mtu fulani anakwabia amefanikiwa katika biashara fulani hivyo na wewe ukifanya utafanikiwa. Jambo la msingi kabla ya kuingia kufanya biashara au jambo fulani hakikisha unajifunza vya kutosha kabla hujaamua kuchua uamuzi wa kuwekeza muda, akili na pesa katika jambo hilo kwani vinginevyo utandokea pua. 

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments