Juzi kati nilikutana jamaa angu mmoja hivi anaitwa Frank hili si jina lake halisi, jamaa tulisoma wote shule ya upili yaani sekondari. Tulipaga stori nyingi sana, tukakumbushana habari za shule na viboko vya enzi hizo🤣 .
Baadae nikamuulizia habari ya ndugu yake mmoja hivi alikuwa ametutangulia madarasa kadhaa, nikamuuliza hivi Emmanuel (siyo jina lake halisi) yupo wapi?
Jamaa akanimbia jamaa yupo Brazil kwa sasa ni padri huko Brazil, nikashangaa dah hongera yake maana nimekumbuka waliosoma darasa moja walikuwa wengi sana ambao walikuwa na wito huo ila yeye pekee ndiye kafanikiwa.
Jamaa akanimbia ni kweli, sisi wenyewe tulijua mara baada ya kumaliza kidato cha sita angeenda kusomea udaktari ila cha kushangaza yeye alisema anataka kuwa padri, nikamwambia hamkupaswa kushangaa zaidi ya kumuombea maana huo wito ni kutoka wa Mungu.
Jamaa yangu kasema ni kweli, akaendelea kunisimulia kuhusu huyo ndugu yake, hivi juzi kati na mara kadhaa huwa ananitumia hela kutoka huko Brazil na hela inangia moja kwa moja kwenye simu.
Nikasema weeeh, kumbe...hapo ndipo nikataka kumchallange baada ya kuniambia huwa anatumiwa hela na huyo ndugu yake Padri kutoka Brazili, nikamuuliza wewe saizi akikupigia simu akisema umtumia shilingi 2,000 je unaweza kumtumia?
Jamaa akasema ndiyo naweza, nikamuuliza utatumia njia gani ili kumtumia hiyo shilingi 2,000? ili naye apate kwenye simu kama ambavyo huwa anakutumia wewe?
Jamaa akasema nangia kwenye menyu ya kutumia hela kama kawaida. Nikamwambia haya sawa ingia unioneshe jinsi utakavyotuma hiyo hela.
Kweli bhana jamaa akachukua simua yake akanza kubonyeza nyota 150 akaweka tena nyota akaweka namba ya mtandao fulani siwezi utaja hapa maana hawajanipa hela😂 kuwatangazia biashara yao.
Jamaa akaendelea kipengele cha kutuma hela, kisha akaenda kwenye namba iliyoandikwa tuma hela kwenye mataifa mengine, kisha akaanza kutafuta nchi ya Brazil ambayo haikuwepo kwenye listi.
Nilikuwa namwambia afanye kisha anioneshe kwani nilijua fika hiyo nchi haipo kwenye nchi ambayo unaweza kutuma hela.
Mwisho jamaa angu akakubali aaah kweli bhana nchi ya Brazil haipo, mwishowe akaachana na kufanya miamala, nikamuuliza je ina maana huwezi kumtumia jamaa hela akiwa Brazil? Jamaa akajibu ndiyo.
Mwishowe tukahitimisha maongezi yetu, huku mimi nikimwambia kuwa sisi watanzania wengi hatupendi kujifunza vitu muhimu kama hivi, ninachotaka kukwambia ni kuwa kumtumia huyu ndugu yako hela akiwa Brazil inawezekana, nenda kajifunze baada ya wiki uje uniambie kama umefanikiwa kujua njia hiyo!
Kweli, baada ya wiki akaja kunielekeza kuwa amefanikiwa kujifunza na akanionesha kwa vitendo kuwa inawezekana!
Chukua hii.
Msomaji wa mafanikio app usikae kinyonge kwa kuamini kila kitu hakiwezekani bali anza kujifunza vitu vyenye tija. Kila kitu kinawezekana endapo utawekeza kwenye kujifunza.
Changamsha ubongo kwa hili.
Mimi Benson, kila mwezi huwa nalipwa mshahara na facebook, Utauliza kivipi? endelea kujiuliza ila huo ndiyo ukweli kila mwezi ikifika tarehe 21 mshahara kutoka Meta huwa unangia moja kwa moja kwenye akaunti yangu ya benki. Mwingine atauliza je unauza nini mpaka ulipwe mshahara? Jibu ni kuwa siuzi bidhaa yeyote ila na wewe nenda kajifunze ili uanze kulipwa na wewe! Maisha yanataka ujifunze ndugu yangu.
(Nb) Sijaandika hili ili kujisifia, ila nataka ujifunze matumizi sahihi ya baadhi vitu ikiwamo mitandao ya kijamii kwani inalipa sana.
Kwa leo niishie hapo.
Tukutane kwenye The diary nyingine, maana ukweli huwa hauipiwi nyundo.
Imeandikwa nami Benson Chonya, afisa mipango.


0 Comments