Ipo hivi, wakati unapochelewesha kufanya mambo ya msingi, unaweza kujisikia vizuri kwa muda mfupi, lakini utaumia kwa muda mrefu. Hivyo kitabu hiki kinaangazia umuhimu wa kuchukua hatua stahiki sasa pasipo kuwa mtu wa kughairisha kufanya mambo ya maingi sasa, pia kitabu kinatutaka tusiwe watu wa kughairisha kufanya mambo.
Haya hapa ni mafundisho 5 kutoka kwenye kitabu Do It Today: Overcome Procrastination, Improve Productivity, and Achieve More Meaningful Things kilichoandikwa na Darius Foroux:
1. Chukua hatua sasa. Foroux anasisitiza umuhimu wa kuchukua hatua mara moja kwenye majukumu na malengo badala ya kuyachelewesha. Anadai kwamba kuendelea kutochokua hatua kwa wakati huongeza msongo wa mawazo na wasiwas wa kutochukua hatua kwa wakati. Ikiwa unataka kupata msukumo wa kufanya jambo lenye tija anza kufanya le. Usiwe mtu kughairisha sana anza kufanya sasa jambo lako.
2. Gawa majukumu kwenye hatua ndogondogo. Kitabu kinapendekeza kugawa majukumu kwenye hatua ndogondogo zinazoweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kutimiza lengo lako kuu. Weka utendaji wako kwenye hatua ndogo, kwamba mwezi fulani hadi mwezi fulani natakiwa kufanya hili, ukifanya hivi utakuwa umeweka utendaji wako kwenye hatua ndogondogo. Kufanya hivyo huongeza motisha za utendaji pia hukusaidia kujua muelekeo wako.
3. Ondoa vikwazo. Foroux anasisitiza athari mbaya za vikwazo ambavyo vitakuondoa kwenye uzalishaji na umakin wako. Anahimiza wasomaji kutambua na kuondoa vikwazo, kama vile matumizi ya iliyokithiri isiyokuwa na tija ya mitandao ya kijamii, kufanya mambo mengi yasiyo ya msingi kwa wakati mmoja. Mwandishi anatutaka kujenga mazingira yanayofaa yatakayotusaidia umakini utaokuongezea kuboresha uzalishaji na ufanisi wako kwenye kazi.
4. Jikite kwenye mambo muhimu. Kikawaida akili ya mwanadamu imeumbiwa kuchoka, hivyo mwandishi wa kitabu hiki anasisitiza kuwa kabla akili haijachoka basi haikikisha unafanya jambo la muhimu mapema. Kila wakati kuwa mtu wa vipaumbele kwenye utendaji wako wa kazi, vipaumbele hivi lazima viangalie yale yaliyo ya muhimu kwenye utendaji, huku yale yasiyo ya muhimu yakiwa mwishoni kabisa kwenye suala la utendaji.
5. Fanya yale yanayokupa mafanikio. Mwandishi anasisitiza kuwa endapo tunataka kufanikiwa zaidi na zaidi basi jikite zaidi kuwekeza fikra na mawazo yako kwenye yale yanayokupa mafanikio. Yale ambayo hayana mchango wowote kwenye maisha yako ni vyema ukaachana nayo mapema kwani hayana maana kwako zaidi ya kukupotezea muda tu.
Kwa kweli kitabu hiki kimejaa wingi wa maarifa ambayo yanachochea umuhimu wa kufanya leo unavyoweza kutupa nguvu na hamasa za kiutendaji kwenye mambo mbalimbali ya msingi ambayo ndiyo chachu ya mafanikio ya kila mmoja wetu. Pia kinaaelezaa namna juhudi zako zitakavyokusaidia kukupa matokeo chanya hasa pale utakavyojitoa kufanya kazi zako kwa ufanisi.
Kitafute kitabu hiki ili uweze kusoma mwenyewe yale mengine ambayo hapo juu sijayakusia kabisa.
Tukutane kwenye uchambuzi mwingine siku ya jumapili saa tisa kamili.
Ndimia afisa mipango Benson Chonya.
Bonyeza hapa kuwasiliana nami.
.jpeg)
0 Comments