Binafsi napenda sana kutumia mtandao facebook kuliko instagram, japo wanasema kuwa facebook ni mtandao wenye utoto mwingi kwa maana ya watumiaji wake...ila huwezi amini mimi napenda sana mtandao wa Facebook ipo siku nitaaeleza kwa kina kwanini napenda zaidi mtandao huo.
Siyo kwamba instagram situmii kabisa, hapana huwa natumia ila ni mara moja moja sana, sasa ngoja nikupe stori fulani niliyowahi kukutana nayo huko instagram.
Siku moja katika pekua pekua zangu, nilikutana na jamaa mmoja amefungua account, ambayo inajihusisha na uungaji wa vifurushi vya bando (internet bundle) kwa bei ndogo.
Nikampekua yule jamaa, baadaye nikaona meseji zake nzuri alizoziandika za kitu anachokifanya, pia nikasoma komenti ambazo watu wanamshukuru kwa kuungiwa vifurushi hivyo anavyovitangaza.
Basi bwana, na mimi nikachukua namba ya yake ya whatsApp nikamtumia meseji huko WhatsApp kwamba nahitaji kifurushi, yule jamaa akanishushia meseji za kutosha kuhusu bei za vifurushi na gb zake kwa mbele pia akaweka gb hizo zinadumu kwa muda gani.
Baada ya kusoma, nikachagua kifurushi nilichokipenda kulingana na pesa niliyonayo, jamaa akasema nakutumia namba ya malipo ili ulipie kifurushi ulichochagua, akanitumia namba ya malipo, lnikafanya malipo kisha nikamjulisha jamaa kuwa nimekwishalipia, akasema sawa nimeona.
Nakuunga sasa hivi, ila kwa kuwa sasa umekuwa mteja wangu, ukileta mteja mwingine utakuwa unalipa kifurushi chochote ukitakacho kwa nusu bei, moyoni nikajisemea yes, hili si dili sasa. Nikaanza kuwafikiria watu ambao wanateseka na ishu ya bando ili niwakutanishe na huyo jamaa.
Kumbuka hapo bado hilo bando sijaunganishwa, wakati nikiendelea kuwawaza watu wengine wanateseka na ishu za bando, huyo jamaa akasema nitumie namba ambayo unataka nikuungie hilo bando...
Bila kupoteza muda nikatuma hiyo namba haraka....yule jamaa akanitumia kapicha fulani kameandikwa loading, kana mstari wa blue hivi akasema subiri kidogo sasa hivi bando litangia kwenye simu yako...nikasema sawa.
Nikaa kama dk kumi, sioni hilo bando likiingia kwenye simu yangu....nikamua kumcheki huyo jamaa, kumbuka hapo tulikuwa tunachati tu.
Nikamuliza mbona sijapa hilo bango? Jamaa hakujibu meseji, nikakaa kama nusu saa hivi nikamtafuta tena, hakujibu na kuanzia hapo blue tick ikawa imetoweka, kumbe jamaa ameshanipiga/ ameshanitapeli na kuanzia hapo akawa ameniblock na hela yangu ikawa imeenda bure kabisa.
Nikaa kama wiki hivi, nikamtafuta tena yule jamaa kwa namba yangu nyingine ili nimpe ukweli wake. Ila nikamtafuta kwa njia ile ile ya mwanzo kama nataka bando, jamaa kama kawaida akashusha bei za vifurushi kama kawaida yake, kisha akaniuliza unataka kifurushi kipi? Baada ya hapo nikamwambia Bro una akili sana juzi kati umenipiga hela yangu...
Jamaa akatuma emoj za kucheka🤣🤣😂 kisha akasema, mwanangu hapa mjini bila ujanja ujanja kula inakuwa ngumu sana, hebu bro fikiria nimemaliza Degree yangu ajira hamna, na nilipomaliza form six nilienda mpaka JKT kwa mujibu wa sheria, lakini yote hayo nimeambulia patupu wewe ulitaka nifanye kazi gani kama si hii?
Nikajikuta na mimi nimecheka😂😂😂 nikamjibu Dah, ila una akili sana maana sijawahi tapeliwa kizembe kiasi hiki, jamaa akatuma meseji pole sana kaka ila asante kwa hela yako🙏.
Nikabaki nimetabasamu maana sikuwa na wa kumlaumu zaidi ya kuwa ni ujinga wangu ndiyo chanzo ya hayo yote.
Chukua hii.
Mara nyingi watu wengi tunapaliwa kwa sababu ya tamaa zetu, tunapenda vitu vizuri kwa bei ndogo, au tunatapeliwa kwa sababu ya tamaa ya kutaka kupata kitu chenye thamani kubwa kwa bei ndogo.
Ndugu yangu, ili uwe salama na utapeli unaoendelea hivi sasa, uwe ni utapeli kama ambao nimetapeliwa mimi au wa aina yeyote ile acha tamaa vinginevyo utakuwa unatapeliwa kila wakati.
Asante kwa kusoma The diary, maana ukweli haupigwi nyundo.
Ndmi Benson Chonya.

0 Comments