Juzi kati nilikuwa kwenye mishemishe zangu za kila siku, mara simu yangu ikaita ilikuwa ni namba ngeni kwenye simu yangu, nilikuwa kwenye kelele nikapokea simu.
Mzungumzaji alianza hallo...
Nikaitikia hallo...akanisalimia habari yako, nikamjibu salama kabisa sijui wewe..akajibu nzuri..ilikuwa ni sauti ya mdada...
Wakati nikiendelea kuwa kwenye kelele...nikaweka simu vizuri ili niweze kumsikia vizuri mzungumzaji.... Akaniuliza bila shaka naongea na Chonya.. nikamjibu ndiyo.
Akajitambukisha jina lake ambalo silikumbuki akasema yeye yupo mkoa fulani hivi upo kanda ya ziwa huko.
Akaendelea kuongea yule dada...akasema mimi nipo sehemu fulani akaitaja, tuhusika na masuala ya afya.
Nikamjibu sawa... Huku maskio yangu yakiendelea kumsikiliza
Akaniuliza wewe upo mkoa gani? Nikamdanganya maana hilo swali ukija kichwa mara nyingi huwa sisemi ukweli😃
Akaniukiza una elimu gani? Hapa nikaguna kimoyomoyo, mtu simfahamu elimu yangu anataka ya nini? Hapa pia nikampa za kichwa kama zile za Mandonga mtu kazi😂 nikwambia nimeishia kidato cha nne.
Akajibu sawa, kabla sijameza mate akaniuliza tena swali jingine, una miaka mingapi, nikajiuliza tena ...huyu dada anataka nini?, nikamdanganya tena nikamwambia nina miaka 25.
Akajibu tena sawa kaka Chonya, nikiwa bado simu ipo sikio nikapigwa swali jingine, una fanya kazi gani? Hapa kidogo nikaamua kumjibu uwongo unaofanana na ukweli, nikwambia nafanya biashara.
Akasema je unaweza kusafiri kuja huku nilipo kufanya kazi nasi? Nikamwambia hapana...hapa sikuwa na konakona nikamjibu mapema bila kusitasita maana alikuwa ameshatibua kwa maswali yake bila yeye kujua.
Akasema basi sawa, naomba unitumie majina ya watu na namba zao za simu ulionao kwenye simu yako. Nikamjibu sawa nakutumia sasa hivi, baada ya hapo akakata simh... nikatulia zangu nikanywa maji, maana maswali yake yalifanya nipatwe na kiu ya ghafla..
akapiga simu kama mara tatu hivi sikupokea, akaendelea kupiga.. nikaamua kumblock.
Chukua hii.
Huenda dada alikuwa na lengo zuri la kunishawishi ili niingie kwenye biashara wanayofanya ila njia aliyotumia ya kuniuliza maswali ya ndani zaidi yaliyonitoa kwenye reli na yalimfanya asipate kitu alichokuwa anataka.
Yawezekana yeye alihisi yupo sahihi kuniuliza maswali sijui ya elimu, umri ila kwa upande wangu nilimtoa kwenye aina ya watu ambao wapo kwenye watu makini kwangu kwenye suala la kutafuta wateja. Hivi unamuulizaje mtu maswali kama hayo mtu ambaye humfahamu? Je unadhani atakupa ushirikiano kweli? Bila shaka sidhani kama utapewa.
Ipo haja ya kujifunza mambo ya msingi wakati wa kufanya marketing, usiulize maswali ambayo yatamtoa mtu kwenye mstari, ni vema ukajielezea wewe zaidi na kile unachokitoa, kisha uende kwenye dhumuni lako la kupiga kuliko kutaka kujua taarifa za mtu usiyemfahamu.
Ongeza na hii:
Wapo wale wengine unakuta unakutumia meseji whatsapp mara ooh bonyeza hapa utapata Gb 20 ya kuperuzi mitandaoni buree. Wakinitumia msg kama hiyo huwa nauliza vipi wewe umepata hiyo Gb 20, utashangaa hawajibu.
Au wale 𝐇𝐄𝐋𝐋𝐎 👋
Naitwa: *PAULIN* ⭐*
Naishi * Mwanza*
𝐍𝐚𝐨𝐦𝐛𝐚 𝐮𝐬𝐚𝐯𝐞 𝐧𝐚𝐦𝐛𝐚 𝐲𝐚𝐧𝐠𝐮
nami 𝐬𝐚𝐯𝐞 𝐲𝐚𝐤𝐨
𝐊𝐰𝐚 𝐚𝐣𝐢𝐥 𝐲𝐚👇👇
📌. Friendship 👥
📌. Kuhabarishana📱
📌 Kupeana connections na updates mbali mbali za kazi📲
📌 Status viewer
NAOMBA NIJIBU KWA JINA LAKO NIKUSAVE 😋
Hawa nao, wakinitumia meseji kama nilikuwa nakula, huwa naacha kula maana huwa wananichefua sana. Inakuwaje unatumia meseji kama hiyo kumbe hinifahamu?
Kwa leo naomba niishie hapa, tukutane kwenye the diary nyingine maana ukweli haupigwi nyundo.
Ndimi afisa mipango Benson chonya.
Je na wewe kitu gani kinakukeraa?, andika hapa kwa kubonyeza hapa ili tuweze kuwaambia ukweli.

0 Comments