Kitabu cha "Diary of a CEO" kilichoandikwa na Steven Bartlett kinatoa mafunzo mengi muhimu kuhusu uongozi, biashara, na maisha. Hapa kuna mambo kumi ya kujifunza kutoka kwenye kitabu hicho:
1. Kitabu kinaeleza kwa kina juu ya changamoto ya uongozi wa kisiasa. Pia kimeeleza ukweli wa maisha ya uongozi ambayo wengi tumekuwa hatuufahamu. Huku suala la uwajibaki wa mtu binafsi likitiliwa mkazo zaidi, mwandishi anasisitiza kwamba tunapaswa kuwajibika sisi wenyewe pasipo kuwajibishwa. Kila mmoja atumbue majukumu yake na kuwajibika vyema katika majukumu hayo.
2. Mwandishi Steven anasitiza hasa suala la kujiamini. Kujiamini huenda sambamba na kuwa na imani thabiti juu ya jambo fulani. Pamoja na ugumu na changamoto ambazo umekuwa ukizipitia kumbuka mafanikio yapo na yanapatikana pia hata kwenye mazingira magumu hayo. Maisha haya yanatutaka sana tuendelee kupambana pasipo kuchoka pia tuendelee kuamini kwenye mawazo yetu hadi pale mawazo hayo yatakapokuwa kitu halisi.
3. Je wajua kuwa makosa ni sehemu ya darasa? Kama ulikuwa hujui basi sasa unapaswa kuelewa kukosea ni shule mpya itakayokusaidia kuweza kufanikiwa zaidi. Mwandishi wa kitabu hiki anasema makosa ni sehemu ya safari ya kuelekea mafanikio yako. Unapopata changamoto kumbuka kujifunza kutoka kwenye makosa hayo ili uweze kufanya jambo kwa ufasaha zaidi. Makosa ni sehemu ya shule hivyo usiogope kukosea.
4. Kitabu hiki kinafundisha umuhimu wa kuwajibika kwenye maisha yako, kwani hakuna mtu mwenye jukumu la kuwajibika kwenye maisha yako isipokuwa wewe mwenyewe. Kuwajibika huku ni lazima kuendane na kufanya maamuzi sahihi ambayo yatakusaidia wewe binafsi kwa namna moja ama nyingine ili uweze kutimiza malengo yako binafsi. Daima unapaswa kukumbuka mafanikio huenda kwa mtu ambaye anawajibika.
5. Ushari mkubwa ambao anatupa mwandishi wa kitabu cha Diary Of CEO ni kujenga mtandao mzuri wa kuaminika. Ambapo mwandishi anashauri kwamba tunapaswa kuwa na uhusiano mzuri na watu muhimu watakaokusaidia katika safari yako ya kimafanikio. Kila mmoja wetu anapaswa kuwa na jicho la ziada litakalomsaidia kuweza kubaini aina hiyo ya watu ili aweze kushirikiana nao vyema kwenye mambo ya muhimu.
6. Mwandishi anasisitiza suala muhimu ambalo litakusaidia kuwa bora zaidi kila iitwapo leo. Pia anashauri kila mmoja aendelee kupambana bila kukataa tamaa kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwani juhudi za kufanya kazi kwa bidii huleta mafanikio makubwa. Pia unafanya kazi basi ni vyema ukahakikisha unafanya kazi kwa kufuata malengo uliyojipangia wewe mwenyewe.
7. Kujenga uongozi wa kuhamasisha, kitabu hutoa mwanga juu ya sifa za uongozi wa kuhamasisha ambao husukuma wengine kufikia mafanikio. Hivyo ukisoma kitabu hiki kitakupa mwangaza mzuri kuwa kiongozi bora huwa na sifa zipi, hivyo ili na wewe ili uwe kiongozi bora na ili uweze kufanikiwa ni lazima uwe na sifa hizo.
8. Kujitathmini, Steven anahimiza umuhimu wa kujitathmini mara kwa mara ili kuendelea kukua na kuboresha kama kiongozi na mtu binafsi. Kwenye hili weka utaratibu kila baada ya muda fulani ili uweze kujitathimini ili kujua kama unakua ama laah. Usipokuwa mtu wa kujifanyia tathimini utakuwa unaishi kama mnyama wa porini tu asiyekuwa na malengo yeyote yale.
Hayo ni baadhi tu ya mambo muhimu ya kujifunza kutoka kwenye kitabu hicho cha Steven Bartlett, "Diary of a CEO". Tafuta kitabu hicho ili uweze kujifunza zaidi na zaidi.
Tukutane tena kwenye uchambuzi mwingine siku ya jumapili ijayo Saa tisa Alasiri....Ishaaalah
Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya!
0747030303
.jpeg)
0 Comments