![]() |
| The Diary (ukweli haupigwi nyundo) |
Ukiniita Afisa Mipango Benson Chonya nitaitika. Mwaka 2019 nilipata wazo la kutaka kuanzisha app yangu binafsi ambayo huko nitakuwa naposti makala ambazo nilikuwa napost kwenye mitandao yangu ya kijamii.
Hivyo nikaanza kutafuta jina lipi litafaa kwa ajili ya app hiyo, nilipata majina mengi sana mwishowe mimi pamoja na marafiki zangu kadhaa tukapendekeza app hiyo itaitwa Mafanikio App, mchakato wa kupata jina hilo halikuwa ni rahisi ulikuwa mgumu sana kwa kweli.
Baada ya kupata jina, nikakaa mbele ya computer yangu na kuanza kutengeneza logo ya mafanikio app. Mchakato wa kupata logo na rangi ipi itumike, mchakati huo hakuwa rahisi pia kama ilivyokuwa kwenye kutafuta jina la app.
Baadae nikaja kupata logo hiyo kama inavyonekana hapo chini. Kumbuka hakuwa mchakato wa muda mfupi.
Mwaka 2020 nikawaza tena na timu yangu, je tufanye nini baada ya kupata jina na logo kabla hatujaanza mchakato wa kutafuta mtu wa kututengenezea app yenyewe?
Master mind, rafiki yangu wa muda mrefu pia Mr Elias, akasema tutengeneze kitu ambacho tutakigawa bure kwa watu na taasisi mbalimbali ili baadae app yetu ikiwa tayari iwe rahisi kufahamika kiurahisi.
![]() |
| Flash za Ben Disk zikiwa zimekamilika |
Baada ya kuchakata sana ni kitu gani tutengeneze kwanza basi mwishowe tukaamua kutengeza Flash disk. Pia ikapendekezwa kwenye flash hizo ziwe na jina langu kama mkurugenzi, pia kuwe na logo ya hiyo app ijayo, bila kusahau tuandike hizo flash slogan ya hiyo app ( Change your Dream into reality).
Tukaendelea na mchakato wa kuwaza pia kuhusu hiyo flash iwaje, tukashauriana kwa kuwa lengo ni kuwagawia watu wa kwenye taasisi na watu wengine bure, tukaamua kudesign flash iwe ni kama kitambulisho cha taifa au cha kupigia kura huku tukizingatia ukubwa ule ule.
Tukawaza kwanza flash yetu iwe ni rahisi kubebeka ambapo mtu akiamua kuweka flash hiyo kwenye walett yake mara baada ya kuitumia iwe inatosha kwenye wallet au pochi yake.
Angalia flash hiyo kwenye picha.
![]() |
| Flash zikiwa kwenye designing |
Mwaka huo huo 2020 mwisho tuagiza flash hizo n China kiwandani zikaja tukaanza mchakato wa kuzigawa bure kabisa kama ambavyo tulikuwa tumeadhimia, tuligawa mwishowe watu walizipenda sana kwa sababu zilikuwa ni nzuri sana, zilikuwa na muonekana wa utofauti na zile ambazo watu wamezizoea kuziona kila siku.
Pia flash zilikuwa na speed kubwa ya kuhamisha vitu kutoka kwenye computer kwenda kwenye flash (speed yake ilikuwa ni 3.0), mbali na yote zilikuwa ni original sana na hilo tulisisitiza kwa watengenezaji (watu wa kiwandani waweze kulizingatia hilo).
Malengo yetu yalikwenda kama vile tulivyopanga, mpaka app inaanza mwaka 2021 mwanzoni ilikuwa ni rahisi kuwashawishi watu watumie app maana tulikuwa tumeshajenga kitu fulani mioyoni mwao na hilo ndiyo lilikuwa lengo letu.
![]() |
| Mafanikio app ikiwa imekamilika. |
Chukua hii.
Mchakato wa kutengeneza flash zenye majina yangu na brand ya app liliwashangaza wengi sana, hivyo nikaona kuchukua kama fursa ya wao kushangaa basi mimi niifanye kama biashara.
Nikaanza kuwatangazia watu kama wanahitaji flash na memory card zenye majina yao, basi mimi nitawatengenezea na kuwauzia kwa bei ya jumla, wateja wakasikia na kuitika ipasavyo, hivyo wengi wa wafanyabiashara na taasisi wanaenjoy sana biashara zao kupitia aidea yangu ambayo nilianza nayo kabla ya kuanzisha app hii.
Hivyo hata wewe kama unahitaji flash au memory card zenye majina yako, au jina la biashara yako nakusihi sana uweze kuwasiliana nami kwa nambari hii 0747030303 au bonyeza hapa ili tufanye jambo litalokutengeneza pesa.
Nb: Flash unaweza kuchagua ni aina ipi unaitaka siyo lazima iwe kama hiyo aidea yangu mimi.
Badili hiki ulichokisoma leo, kwa kuchukua hatua.
Tukutane kwenyeThe diary nyingine maana ukweli hauwezi kupigwa nyundo. Asante na kila lenye kheri kwako.



.png)
0 Comments