Ubora pekee katika maisha yako hujengawa na wewe mwenyewe na namna ambavyo hutumia muda wako mwingi kutafakari kuhusu wewe.
Namna pekee itakayokutofautisha na watu wengine katika ulimwengu huu itatokana na vile ambavyo umekuwa ukiutumia muda mwingi kwenye kutafakari jinsi na namna ambavyo unatakiwa kuwa.
Katika hili unashauriwa walau kila siku utenge masaa kadhaa kwa ajili ya kuwaza na kuwazua ni kwa namna gani utakuwa bora zaidi kwenye mambo uyafanyayo au unayotaka kufanya.
Katika hili unapaswa kufikiria namna ambavyo kila wakati unapaswa kuwa bora zaidi ya jana, ukifanikiwa katika hili utaona mabadiliko makubwa ambayo mwanzo ulikuwa huyaoni.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.
0 Comments