Ukienda polisi wanaita dhamana.
Ukienda msibani wanaita rambimbi
Ukienda shuleni wanaita ada.
Ukiajiriwa wanaita mshahara
Ukistaafu wanaita mafao.
Ukitaka kulipia maji au umeme wanaita billi.
Ukienda hospitali wanaita bill pia.
Ukiazima kitu bila kuwa nayo wanaita mkopo.
Ukienda kwenye mashindano wanaita tuzo.
Kama umepanga nyumba wanaita kodi.
Ukienda mahakamani wanaita faini.
Ukienda kanisani wanaita sadaka.
Ukitaka kuoa wanaita mahari.
Ukienda serikalini wanaita kodi.
Ukisafiri wanaita nauli.
Nyingine ongeza mwenyewe ....
Ila unachotakiwa kujua ni kuwa unatakiwa kuwa na hela kwa sababu kila kitu kinahitaji fedha ndugu yangu, haya majina yasikuchanganye bali hayo yote yanahitaji fedha yako endelea kupiga kazi ili umiliki fedha.
Ndimi: Benson Chonya.

0 Comments