BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Tumia Kanuni Hii, Utafanikiwa.

 


Moja ya kanuni kubwa ya kimafanikio ambayo unatakiwa kuanza kuitumia ni KUKATAA KUTOA SABABU YOYOTE. Kama kuna kitu unakifanya, kifanye. Kama kuna kitu umeshindwa kukifanya huna haja ya kuendelea kutoa sababu kwa nini umeshindwa. 

Acha kutumia ubongo wako hovyo kwa kutoa sababu. Uelewe sababu unazozitoa hata ziwe nzuri vipi haziwezi kukusaidia. Unataka kufanikiwa, usiendelee tena kutoa sababu kwenye maisha yako, NO MORE EXCUSE IN YOUR LIFE.

Watu wanaoshindwa ni watu wa kutoa sababu kila siku. Watu wa mafanikio ni watu wa kuchukua hatua. 

Jiulize au waangalie wale wote wanaotoa sababu kama wewe, kuna mafanikio ambayo wamepata? Ukiangalia, hakuna mafanikio waliyopata. Hiyo ni ishara tosha kama unaendelea kutoa sababu pia ni ngumu kuweza kufanikiwa.

Ukikubali kweli leo, kutumia kanuni ya kutokutoa sababu, hakika amini utatimiza ndoto zako nyingi na utafanikiwa.

Makala hii imeandikwa na Melisa Kawa wa Dar es salaam, Tanzania.


Mawasiliano; 0745268398.

Post a Comment

0 Comments