Ni ngumu sana kwa watu wengi kulinda uzito walionao usiongezeke, lakini zoezi hilo ni rahisi sana kuliko kuambiwa upunguze uzito.
Ni shida na ngumu kwa watu wengi kuambiwa wabadilishe mafuta au oil za gari zao, lakini zoezi hilo ni rahisi sana kuliko uambiwe ubadilishe injini nzima.
Ni ngumu pia kwa wengi kula vyakula vya afya, lakini zoezi hilo ni rahisi sana kuliko kuambiwa usile chakula hiki au kile kwa sababu kwa sasa una kisukari.
Watu wengi huwa wanashindwa kulinda vile vitu walivyoonavyo hata kama ni kwa gharama ndogo wanashindwa kuvilinda, na matokeo yake wanavipoteza.
Acha kuwa na tabia ya kutokuvitaka au kuchezea vitu ulivyonavyo kama afya, mali au ujuzi wako. Kama hutavitaka leo, utakuja kuvutumia baadae. Maisha ni rahisi kama utakuwa unalipa gharama zinazostahili kwa jinsi unavyokwenda. Lipa gharama za kutunza vitu vyako ili visiharibiwe au kupotea.
Imeandikwa na Imani Ngwangwalu.
0 Comments