Uchambuzi wa kitabu cha leo ni kitabu cha Oprah Winfrey kinachoitwa What I Know for Sure, ambapo leo nimekusogezea mambo kumi ambayo utajifunza kupitia kitabu hicho kama ifuatavyo:
1. Mwandishi Oprah anasema ili uweze kuwa mtu mwenye furaha katika maisha yako basi jifunze mambo makubwa mawili. Mosi jifunze kuwa mkweli na jambo la pili jifunze kuwa mwaminifu. Ukifanikiwa kuwa na mambo haya makubwa mawili neno furaha katika maisha yako halitajitenga nawe.
2. Mtazamo mzuri wa kimaisha ya mtu binafsi hujengwa na mtu mwenye shukrani. Huwezi kuwa na mtazamo mzuri kama utakuwa si mtu shukrani, hivyo jifunze kuwa shukrani kwa kila jambo. Shukuru kwa kila jambo ili baraka za mafanikio zizidi kuwa nawe siku zote za maisha yako.
3. Jifunze kujipenda wewe mwenyewe kabla hujaanza mchakato wa kuwapenda watu wengine. Ukijipenda wewe mwenyewe itakusaidia sana kwa namna moja ama nyingine kuwapenda watu wengine pia. Jifunze kujijali kwanza wewe ndipo uanze kuwapenda watu wengine pia, ukifanya hivyo utafanikiwa kujenga uhusiano mzuri na watu wengine pia.
4. Ili uweze kuwa na furaha mwandishi Oprah anasema jifunze kuzifuata ndoto zako na kuzitimiza ndoto hizo. Ukifanikiwa kufanya hilo ni ukweli ulio wazi kuwa furaha itakuwa upande wako na utapata mafanikio yale unayoyataka.
5. Unapopitia changamoto jifunze kitu kutoka kwenye changamoto hizo unazozipitia. Unapopitia changamoto inakufanya kuwa imara kwani inakusaidia kuwa imara sana na kukufanya uweze kukua zaidi na zaidi.
6. Epuka kuishi bila kuwa mipango na melengo, bali jifunze kuwa ni mtu wa kuweka misingi thabiti itakayokusaidia kufikia mafanikio uyakayo. Unapoweka mipango kumbuka kuweka pia njia ya kutimiza mipango hiyo.
7. Kila wakati jifunze kuwa na aina za marafiki chanya, marafiki ambao wanakutia moyo wa kuendelea kupambana zaidi na zaidi na kukusukuma mbele kwenye mambo ya kimaendeleo. Usichague marafiki wakatisha tamaa ambao hawana mchango wowote katika maisha yako.
8. Jifunze kusamehe, unaposamehe unapata amani moyoni mwako, wakati mwingine kusamehe husaidia kuponya majeraha yaliyo ndani yako ambayo yanakufanya usiweze kusonga mbele zaidi. Usikae ni vitu moyoni bali jifunze kuachilia ili uwe na amani na upate nguvu ya kufanya vitu chanya zaidi.
9. Jenga maisha mazuri ya kiroho. Usikae mpweke bali jenga mahusiano mazuri na Mungu wako. Unapokaa karibu na Mungu wako ni kwamba mambo mengi ambayo yalikuwa yamefungwa huwa yanafunguka yenyewe. Usiwe bize kiasi hicho ndugu bali kuwa karibu na Mungu wako.
10. Maisha haya ya kila siku yanakutaka uweze kuwa ni mtu wa kutoa na kujitolea kwa wengine kwani ukifanya hivyo utapata furaha na kufurahia maisha unayoishi. Usiwe mtu wa kupokea tu, bali jifunze kuwa mtu wa kutoa kwa watu wengine ili uweze kubarikiwa zaidi na zaidi.
Kitabu hiki kimeangazia kwa kina namna ya kufanikiwa na kutengeneza furaha ya kweli endapo tu yale yaliyoandikwa katika kitabu hiki utayaweka katika matendo.
Imeandikwa na afisa mipango Benson Chonya.
0 Comments