BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Ushindi maishani hutengenezwa hivi.

U-halisia wa maisha mara nyingi hutokana na vile ambavyo wewe mwenyewe ujionavyo. Kama ndani mwako unajiona kuwa huwezi kufanya jambo fulani basi hata akitokea mwalimu wa kimataifa akufundishe juu jambo fulani, hakika huwezi kuelewa na kufanikiwa katika jambo hilo kwa sababu wewe mwenyewe ndani mwako umekwisha jiona kwamba huwezi.

Hivyo ni muhimu kuelewa ya kwamba kila jambo ili liweze kufanikiwa kwa viwango vya juu basi itatokana na vile ambavyo mtu huyo atakuwa anajiona kutoka nafsini mwake, kama wewe unataka kufanikiwa basi anza kujiona ni  mshindi kuanzia siku leo.

Pia unatakiwa kujinenea yale yaliyo mema yenye kukujenga na kukupa hamasa za kiutendaji kwenye kila jambo ambalo unataka lileta matokeo chanya na maendeleo kwa ujumla. Kabla hujaanza majukumu yako ya siku basi jinene ya kwamba wewe ni mshindi katika jambo fulani na utakwenda kuwa bora zaidi.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments