Watu wengi husema bado najiandaa, na visingizo vingi kama hivyo, watu wote ambao huwa wanasema wanajiandaa mara nyingi huishia kusema tu pasipo kuweka yale wanayoyasema katika matendo.
Elewa wakati mwingine mwenye haki na maisha yako ya mafanikio ni wewe mwenyewe, hivyo unapoamua kufanya jambo fulani wewe anza kulifanya jambo hilo mara moja, haijarishi ni hatua ndogo kiasi gani uliyopo, bali unatakiwa kuanza hapo ulipo.
Anzia hapo ulipo kuelekea katika mafanikio yako, kwani kila wakati kila hatua ya tamu huanza na chachu.
Imeandikwa na Imani Ngwangwalu.

0 Comments