BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Uzuri wa kitu upo kwenye jambo hili.

 


Umeshawahi kujiuliza uzuri wa kitu uko wapi, kama kitu hicho hukitumii ipasavyo?

Uzuri wa mzazi mzuri uko wapi, ikiwa kama huna nafasi ya kukaa karibu na watoto wako?

Uzuri wa maisha uko wapi, ikiwa unaishi vibaya na watu na kuleta mvurugano kila mahali?

Uzuri wa maarifa uko wapi, ikiwa maarifa unayoyapata huyatumii kukusaidia kufanikiwa?

Uzuri wa utajiri uko wapi, ikiwa utajiri huo huutumii kuwasaidia watu wengine?

Mara nyingi uzuri wa kitu, upo kwenye matumizi, kama kitu hicho hukitumii basi hakuna uzuri wowote. Hakikisha  vitu ulivyonavyo, vitumie kwa uzuri ili vikuletee mafanikio bora.

Imeandikwa na Imani Ngwangwalu.


Post a Comment

0 Comments