BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jambo unalotakiwa kulijua siku ya leo.


Haijalishi utafanya nini katika siku ya leo, lakini unatakiwa ujue siku hii ya leo ikiisha utakuwa umechoka tu.

Inawezekana ukawa umechoka, kwa sababu ya juhudi ulizofanya na yale uliyoyafanikisha au unaweza ukawa umechoka kwa sababu ya kutokufanya chochote. Uchaguzi unabaki kwako umechoka kwa kipi.

Inaleta maana sana, kama kweli umechoka kwa sababu ya juhudi ulizoweka, umechoka kwa sababu ya mabadiliko na ubora  ulioufanya, hii inakuwa inaleta picha nzuri ya kweli umechoka kwa faida ya maisha yako.

Inapofika jioni, lazima utahisi eidha, umechoka na kuwa na msongo wa mawazo, au umechoka na kuridhika kutokana na kazi uliyoifanya imekuridhisha. Uamuzi unabaki kwako umechoka kwa kipi.

Kumbuka, kile unachokifanya, ndicho kitatoa majibu ya kwamba, unachoka kwa namna ipi, kama unafanya mambo ya hovyo, utachoka na kuwa na msongo wa mawazo, lakini kama unafanya mambo safi ya kubadili maisha yako, utachoka na kuridhika.

Imeandikwa na Imani ngwangwalu

Post a Comment

0 Comments