Kila maamuzi unayoyachukua, yanaweza yakawa mazuri au yanaweza yakawa mabaya. Kitu cha msingi ni kuwa makini tu kabla hujafanya maamuzi unayofanya wewe, maana kila maamuzi yana matokeo yake.
Kila kitu unachoamua kukifanya, elewa kitu hicho kinachangamoto zake, hivyo kwa kujua hivyo, hutakiwi kurudi nyuma, maana changamoto hizo zipo na unatakiwa uzishinde ili ufanikiwe, kinyume chake, UNAKWAMA.
Fanya uamuzi wa kuchagua kitu unachotaka kukifanya, na kisha kifanye kitu hicho bila kusitasita. Uchaguzi au maamuzi yako yasikuangushe, unatakiwa kuwa makini tu, kwa sababu kila maamuzi yana matokeo yake.
Imeandikwa na Imani Ngwangwalu.

0 Comments