BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Huu ndiyo ulimwengu waishio watu wengi.

Wengi wetu, bado tupo tunaishi kwenye ulimwengu wa NATAKA..

Utakuta mtu anakwambia nataka kununua gari,...nataka kujenga nyumba,...nataka kufanya kilimo,...au nataka hiki au kile.

Wengi ndio bado tupo kwenye ulimwengu huu wa nataka. Ikiwa kweli unataka mafanikio, unatakiwa uhame kutoka kwenye ulimwengu huo na kwenda kwenye ulimwengu wa utendaji.

Nataka kufanya hili au lile, haijawahi kumsaidia mtu, kama mtu huyo hachukui hatua. Kitakachokusaidia wewe ni kuchukua hatua na sio 'nataka' tu peke yake.

Anza kuishi, kwa kuchukua hatua zitakazo kusaidia kutimiza ndoto zako, lakini achana na habari ya nataka.

Mafanikio yako yanakuja kwa wewe kuchukua hatua na sio nataka...kuendelea kujiambia nataka hii au ile itakukwamisha kwenye maisha yako.

Kikubwa kwako, chukua hatua na utayaona mafanikio kwenye maisha yako.

Imeandikwa na Imani Ngwangwalu

Post a Comment

0 Comments