Je, umeshawahi kujiuliza ni kitu gani ambacho kinawapa hamasa na msukumo mkubwa mabilionea hadi kufikia hapo walipo na kuwa na pesa nyingi za kujitunza wao, watoto, na hata wajukuu?Jibu ni rahisi tu, ni maono waliyonayo, ya kutaka kufanya mabadiliko ya maisha yao na maisha ya wengine pia na kuweka alama duniani.
Hicho ndicho kitu kinawasukuma sana mabilionea duniani wawe kama walivyo, Ndio maana, unaona mabilionea wengi, ni watu wa kufanya kazi kwa muda mrefu na hawachoki, hiyo yote ni kwa sababu ndani yao tayari wana maono yanayowasukuma kufanya hivyo.
Hata wewe leo ukiacha kufanya kazi kwa ajili ya kula na ukaamua uwe na maono yako, na ukafanya kazi ili kuleta mabadiliko kwako na kwa wengine, basi utafika mbali sana kimafanikio.
Asante sana kwa kusoma makala haya.
Imeandikwa na Imani Ngwangwalu.

0 Comments