BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Yasema haya kila unapoianza siku yako.

Kila mmoja wetu anapaswa kuwa ni mtu mwenye hekima kwenye matamshi yake, hususani yale anayojiambia yeye mwenyewe. Kuna nguvu kubwa sana ya maneno hasa yale unayojiambia wewe mwenyewe.

Nimesema hivyo kwa sababu wapo baadhi ya watu, wanaishi maisha magumu hii yote kwa sababu wao wenyewe walijinenea mambo ambayo yamewafanya mpaka leo hii wamekuwa na mambo magumu. 

Kwa mfano wapo baadhi ya watu walisema hata iweje hawawezi kufanikiwa! Na kweli mpaka leo watu ukiwatazama watu hao ni kweli hawajafanikiwa, hiyo yote imesababishwa na vivywa vyao.

Ukweli usiopendwa na watu wengi ni kwamba ipo nguvu kubwa sana kwenye maneno hasa yale tunayojiambia sisi wenyewe, hivyo kila wakati tunapaswa kuwa ni watu wenye hekima kwa kujinenea yale yaliyo mema kila siku. Pia tujifunze kujipa nguvu ya utendaji kwa kujinenea yali yaliyo mema kila wakati.

Kwa mfano unaweza kusema kila unapoianza siku yako  kuwa "wewe ni mshindi na utapambana mpaka pale utakapoona maisha yako yakuwa sawa kama vile ulivyopanga". Ukifanya hivyo ni lazima utaona mabadiliko makubwa maishani mwako.

Kila wakati unapaswa kujinenea yale yaliyo mema ili ufanikiwe.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments