BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mara myingi pesa ni sawa na kitu hiki.

Mara zote pesa ni kama kifaa tu cha kutendea kazi fulani, ambapo mtumiaji wa kifaaa hicho unatakiwa kuwa makini kwenye namna ya kutumia kifaa hicho. Kifaa hicho hakina utashi wala uelewa wa jambo lolote lile.

Kifaa hicho chenyewe hufwata maelekezo ya namna kinachopaswa kufanya kazi kutoka kwa mmiliki wa kifaa hicho. Mtumiaji yeye ndiye mwenye hisia za kitu gani kifanyike kwa kutumia kifaa hicho, ila changamoto ni kwamba mtumiaji wa kifaa hicho huendeshwa na hisia zaidi kwenye kufanya matumizi ya kifaa hicho kuliko kutumia akili.

Ukweli ni huu, ikiwa unataka kutumia kifaa hicho pasina matatizo wala kupelekeshwa na hisia hasi kwenye kukitumia kifaa hicho unapaswa kutuliza hisia zako kwenye upande sahihi wa namna ya kutumia kifaa hicho. 

Akili yako inapaswa kuwa na mipango sahihi ili kifaa hicho kinavyofika mikononi mwako kiende moja kwa moja kwenye utekelezaji sahihi, epukana na kutokuwa na mawazo ya namna gani kifaa hicho kinatakiwa kufanya kazi hasa pale ukipatapo, kwani ukifanya hivyo ni lazima kifaa hicho kitakupelekesha tu, kwani kama nilivyosema hapo awali kifaa chenyewe hufuata maelekezo kutoka kwa mmliki.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments