Wapo baadi ya watu wanashindwa kufanya mambo makubwa kwa sababu bado wanaishi nyuma yao, wengi wao wanaishi katika maumivu na mashaka waliyowahi kukutana nayo kipindi cha nyuma, Hili ni jambo si jambo la muhimu sana maishani mwako kwa sababu kendelea kuishi maisha yako ya nyuma uliyoyapitia ni kuendelea kujirudisha nyuma mwenyewe kimaendeleo.
Hii ni kwa sababu wapo baadhi ya watu wanashindwa kufanya mambo mengine mapya eti kwa sababu kipindi cha nyuma waliwahi kufeli kwenye jambo fulani. Hivyo ikiwa unataka maisha mazuri yenye furaha na mafanikio tele ndani yake unapaswa kuyaacha yale yote yaliyopita yasiwe kikwazo cha kukuzuia kufanya mambo mapya.
Yale tote uliyowahi kuyapitia yasiwe giza kwenye kufanya maamuzi mapya, bali yote uliyoyapitia yabaki kuwa ni histori tu, kwa sababu bado unayo nafasi ya kufanya mambo mengine katika ukubwa uutakao wewe, hivyo kwenye maisha haya ya kila siku, haijalishi ni magumu kiasi gani umepitia unapaswa kuishi katika usemi wa yaliyopita si ndwele, tugange yajayo.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.

0 Comments