BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Dhana sahihi ya fedha isiyoijua.

Dhana sahihi ya pesa ndiyo ambayo huwatofautisha matajiri na maskini. Matajiri huwekeza fedha kila wazipatapo, huku maskini huwaza kutumia pesa badala ya kufanya uwekezaji. 

Pia kile unachokijua na kile unachokifanyia kazi kuhusu kile unachokijua ndicho kitachokupa dhana sahihi kuhusu pesa. 

Kwa mfano, kama unachokijua kuhusu pesa kwamba ni za watu wachache ni kweli hata wewe pesa hizo hazitakuja kwako kwa sababu utabweteka na kuwaachia wale wenye bahati ndiyo wazipate. 

Ila kama ikiamini kuwa pesa ni za watu wote ni rahisi sana kuweza kuzipata kwa sababu utawekeza muda wako mwingi kwenye kufikiri namna ya kuzipata fedha hizo.

Hivyo unapaswa kuwaza chanya ili uweze kupata dhana sahihi kuhusu pesa, kwani ukifanya hivyo utakuwa na mtazamo sahihi kuhusu pesa, na pesa hizo zitakuwa upande wako. 

Pesa ni za watu wote, jenga dhana sahihi kuhusu pesa.

Waza chanya ili upate maokoto

Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya

Post a Comment

0 Comments